ONDOA WEUSI KWENYE MAGOTI NA MIKONO.
by dr love
Ngozi nyeusi katika magoti na nyuma ya mikono hutokana na mkusanyiko wa
cells zilizokufa, na hata unavyoweka pressure kwenye magoti na vipepsi
vya mikono yako. Kama ukiwa unaweka mikono kwenye meza ukiwa kazini, ule
msuguano unafanya ngozi iwe nyeusi.
Kama una magoti myeusi na nyuma ya mikono pia ni peiusi, tumia hizi njia asili kuweza kuondoa weusi huo::
Tumia Aloe Vera Juice
Juice ya Aloe Vera inasaidia kuondoa weusi, all you have to do ni kupaka
juice hiyo kwenye sehemu yenye weusi na uache kwa nusu saa kisha nawa
na upake moisturizer. Rudia kufanya hivi mara mbili kila siku.
Tumia Binzari Manjano, Asali na Maziwa.
Changanya vyote hivi utapata mchanganiko mzito, paka kwenye magoti na
kwenye mikono yako palipo na weusi. Kaa nayo kwa dakika 30, nawa na paka
moisturizer. Rudia hii kila siku kwa wiki 3-4, utapata matokeo mazuri.
Tumia Ndimu.
Chukua pamba na uitumie kupaka juice ya ndimu katika sehemu zenye weusi.
Au unaweza kuikata tu ndimu na kuipaka directly kwenye sehemu zenye
weusi. Kaa nayo kwa lisaa 1 kisha nawa. Rudia hivi kila siku hadi weusi
utakapopotea.
Chapisha Maoni