0

Ni wazi love clinic FURSA tumejionea kwamba kadri changamoto zinavyozidi kuongezeka siku kwa siku,watu wengi wamekuwa wakifikiria kwa kuangalia nini wafanye ili kujikwamua na kuzidi kutengeneza mzunguko bora wa pesa.Katika kutatua changamoto za maisha kwa kuangalia namna ya kukuza vipato kwa kutumia vile vipato vidogo tulivyonavyo,kumekuwa na changamoto nyingi sana katika biashara za bodaboda.
Bodaboda imekuwa ndio njia ya haraka abiria wanaitumia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.Njia hii ya haraka imeweza kuwa kama njia moja ya ajira kwa vijana wengi katika miaka michache iliyopita.Lakini kadri siku zinavyosogea watu wengi wamekuwa wakiwekeza katika fursa hii,na wengi wamekuwa na sababu mbali mbali zinazowafanya waingie kwenye biashara hii.Sababu hizi ni kama kupewa hamasa na marafiki,au kushauriwa na watu walioko katika makundi na Nyanja mbali mbali.
Lakini wengi wao wanaofanya biashara hii ya bodaboda wamekuwa wakifanya biashara hii kwa kuwapa madereva na kuletewa hesabu kila siku.Njia hii japokuwa inaonekana kupendwa na wengi bado imekuwa ni njia yenye changamoto nyingi sana.Changamoto hizi ni Umanifu,fursatz.com inakiri kuwa kama alivyowahi kusema mwekezaji maarufu duniani Mzee Warren Buffet kwamba umanifu ni zawadi ya gharama na usitegemee kuipata hiyo katika watu warahisi warahisi ni kweli kabisa katika biashara zetu hasa wajasiriamali wadogo wadogo wamekuwa wakikumbana na haya.

Mmoja kati ya wamama wajasiriamali aliyejinyakulia mkataba
Lakini katika kutatua tatizo hili basi ni vyema kabisa kuiangalia fursa hii ya kuwekeza kwenye biashara ya bodaboda kwa njia ya Mkataba.Yaani unanunua bodaboda unaingia mkataba na dereva baada ya muda flani gharama zako za manunuzi jumlisha na faida mliyokubaliana basi pikipiki inakuwa mali yake.Njia hii ni moja ambayo fursatz.com imeona ikitumiwa na wengi wanaofanya biashara hii.
Moja ya faida kuu katika biashara hii ni:
Kuletewa pesa yako mliyokubaliana kwa siku na asipofanikiwa kuipata siku hiyo basi lazma atakuja kuilipa.
Kuepuka gharama za utengenezaji na marekebisho ya pikipiki
Kuondoa lawama za kwamba leo sikupata.
Mara nyingi na wengi wanashauri kwamba nilazma kujilinda kwa mkataba kutoka kwa mwanasheria ili pindi pale tatizo linapotokea uwe na katika upande mzuri wa kuweza fatilia tatizo lako.Sababu hapa pia anayekodishwa atakuwa na wadhamini ambao ni rahisi kuwakamata pindi tatizo linapotokea.
Pia ni vyema kuhakikisha umekatia bima pikipiki yako kwa sababu za kiusalama na kukuepushia gharama pindi unapopata tatizo ama ajali.
AINA ZA PIKIPIKI
Zipo aina nyingi za pikipiki zinazofanyishwa biashara hii ya boda boda,na zinapendwa na madereva wengi.
1. HONDA (Zisizokuwa na starter ya kick)
2. HONDA yenye starter (Rim za Spoku) CC125
3. BOXER CC150
4. FEKON CC125
5. KINGLION CC150
6. SUNLG CC125
Kama fursatz.com ilivyoona madereva wengi na wamiliki wao wanasema Fursa hii ya mkataba inawasaidia, kwasababu dereva anakuwa anawajibika kwa kina sababu anajua baada ya mkataba kuisha umiliki wa pikipiki unakuwa kwake kwahiyo utunzaji wa pikipiki unakuwa wa hali ya juu. Hii inakuwa tofauti na ile aina ya biashara ambayo mmiliki anampa dereva amletee mahesabu kila siku.
UHALISIA WA MAPATO:
1. HONDA YA KICK (MKATABA)
Vijana wengi wanasema mkataba wake unakuwa wa miezi 12 yaani siku 365 na hesabu ya siku ni 15,000/=.Ambayo mpaka mkataba uishe utakuwa umepokea 5,400,000/=.Ila wengine wanasema kwenye HONDA pia wanakubaliana mpaka miezi 12 .Swala hili linakuwa ni makubaliano ya mwenye mali na dereva.
2. SUNLG
Pikipiki nyingi za kichina kama SUNLG hizi ni miezi kumi na moja na hesabu yake kwa siku ni 10,000/= kwahiyo jumla ya miezi 11 unakuwa umetengeneza 3,300,000/=.
Mifano hii midogo umetuwezesha kuona fursa hii ilivyo.Fursatz.com inakiri kwamba ni ukweli usiopingika kwamba walioanza zamani waliweza fanikisha vyema na fursa hii.Hivyo basi kabla ya kuianza biashara hii kufanya utafiti wa kina ili kuepuka au kupunguza hasara kulingana na uhalisia kwamba watu wengi wamekimbilia kwenye biashara hii ni vyema kujiridhisha kiutafiti kabla hujafanya maamuzi yeyote.
Fursatz.com inakumbusha kuwa katika biashara ya boda boda sehemu unayofanyia biashara ina changia sana katika mzunguko wa pesa.Ni kweli sehemu za mijini biashara hii inafaida sana ukilinganisha na sehemu za vijijini,kwa hiyo ni vyema kuhakikisha unafanya utafiti wa kina sehemu unataka wekeza fursa hii ukizingatia na malengo yako kibiashara.

Chapisha Maoni

 
Top