Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndio uanzishe
biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha,Ukweli ni
kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika kuanzisha
biashara,lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo
sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana.Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na
kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria
kuanza kukodi ofisi yako,kuajiri watu wengine nk ,ingawa ni rahisi
kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi Fulani
hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe
umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na
degree ya chuo kikuu.
Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali,workshop
mbalimbali,au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata
ujuzi kuanza fanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa
bora kwa upande huo.
Nimejaribu kuorodhesha aina zaidi ya 14 unaweza
anzisha pasipo kuwa na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana.Hizi ni aina
ya biashara ambazo nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na
nyingine nimeshuhudia watu wakifanya na kufanikiwa.
Kama kweli una shauku la kweli kuanza leo biashara soma kwa umakini
sana na kuona je ni wapi pa kuanzia ili uweze timiza lengo lako la
maisha:
Zifuatazo ni baadhi ya biashara unazoweza anzisha kwa mtaji mdogo sana au pasipo mtaji kabisa:
i. Huduma za kuandika miradi biashara(business plan),kama
ilivyo kwa tafiti za uchanganuzi yakinifu(hali halisi ya
biashara)wajasiriamali wengi huwa huepuka kufanya kazi hii ngumu ya
kuandika mradi biashara(business plan) yao.Ukweli ni kuwa wajasiriamali
wengi hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa kuwashawishi
wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza
kwa hilo.Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.
ii. Mshauri wa mambo ya biashara:Wewe
ni unauzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara?Unajua nini
kinahitajika ili uanzishe biashara,kujenga biashara,kuingoza biashara na
kukua?Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara.Unaweza saidia
kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa
ushauri na maelekezo muhimu.Unaweza kuwasaidi watu walioajiriwa kuanza
kutoka kwenye ajira na kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.
iii. Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu.Wewe
ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara
mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu kwa vya uhasibu(hili ni
jambo huwa na shauku kulipata)? Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe
kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.
iv. Kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha matukio(Event management),kampuni
nyingi kila mara huwa na matukio mbalimbali mfano semina,siku ya
familia,sherehe mbalimbali mara nyingi kampuni kama kampuni haiwezi
kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya,na hivi ndivyo ilivyo
kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika tofauti na kuandaa
matukio ya kampuni na kuyasimamia,hivyo ili kuwa na ufanisi hapa inabidi
kampuni zikodi watu wan je wenye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa
uhakika,wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo
mwanzo mpaka mwisho uwanja ni wako.Mfano kuna matukio kama siku ya
familia,semina kwa wafanyakazi,maonyesho ya biashara ndani nan je ya
nchi kwa kampuni husika nk
v. Kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali,Kwa
afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo steji za
mwanzoni,Unaweza anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu
wanatafuta ,baada kuwa mmiminiko wa watu wengi wanaotembelea tovuti
yako,unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe na
kutengeneza fedha za kutosha.Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti
usijali kuna tovuti za bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari
kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja
unakuwa na wewe tovuti yako,na kama unahitaji nunua domain unaweza
ikawa moja kwa moja tovuti yako.Tovuti unazoweza ingia na kutengeneza
tovuti yako bure niwww.weebly.com,www.webs.com nk au pia unaweza tengeneza blog ikawa ni unaweka taarifa watu wanatafuta na kisha kutafut wadhamini wa hiyo blog.
vi. Mshauri wa masoko,Je wewe unaweza
nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja wangu
kuanzia aslimia 30% -70% au zaidi?kama ndio biashara ipo mikononi
mwako.Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko kwa
wamiliki biashara ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta
wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada Fulani ,kutokana huduma
husika.
vii. Mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa;Kampuni
nyingi za nje zinazokuja hapa nchini,huwa wanahitaji kutafsiri taarifa
zao kwenda lugha ya wazawa,mfano mradi Fulani,tovuti zao,mfano kama ni
kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa ili auze kwa wazawa
inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa,Pia mfano kuna hata miradi
mbalimbali ambayo inatakiwaiangaliwe na wazawa nk.
viii. Kutafiti fursa mpya za biashara,Nina
marafiki wangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi fursa mpya na
wanafanya vema kwenye hii biashara.Wanachofanya kutupia jicho kwa mambo
yajayo,mwelekeo,mahitaji aua fursa za biashara;na kuandaa mradi/mpango
kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa.Wakati mwingine
wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa
moja kubwa la kutosha;na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya
kuayaendeleza.Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa hudumu kutafiti
fursa mpya za biashara
ix. Kutoa huduma za ku-print,Biashara
hii inafahamika sana na wengilakini bado inalipa sana.Unaweza kuanza
kutoa huduma ya ku-print business,banner sposters
card,viperushi,flyers,catalogues kwa biashara ndogo na za kati.
x. Kutoa huduma za kuajiri,Siku
hizi kazi za managementi za rasilimali watu kwa kampuni nyingi hutolewa
na tenda kwa kampuni za nje ya kampuni husika kufanya hiyo kazi ili
kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na hivyo kupelekea kampuni husika
kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake mahususi.Kama una uelewa na
ujuzi wa kutosha wa kushughulika na maswala ya rasiliamali watu uwanja
ni wako,kwa sasa hapa Tanzania kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure
unatakiwa uende pale wizara ya ajira na vijana kujisajili.
xi. Mshauri wa mitandao ya kijamii (social media consultancy),Kwa
hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia kubwa sana.Je wewe
unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya kijamii?Unajua jinsi
ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa(brand) za makampuni ndani
ya mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na linkedin?Basi unaweza
kuwa mashauri wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha zako.
xii. Kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni,Je
wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni?unajua jinsi ya
kuchagua jina sahihi la kampuni?unajua stepu zinazohitajika ili
ukamilishe uandikishe jina la biashara?Anza sasa fungua biashara yako ya
kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni .
Huduma nyingine unaweza fanya ili kutengeneza fedha:
xiii. Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au huduma yako
xiv. Huduma za ushauri kwa biashara ndogo
xv. Kuandika kitabu kizuri na kukiuza kwa umma.
Chapisha Maoni