VIDONDA VYA TUMBO
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao unatokana na kumomonyoka (erosion) au kutoboka kwa tabaka la juu la utumbo.Kwa kawaida tabaka la juu la utumbo hulindwa na ukingo maalum (gastric mucosal barrier) kwa kutengeneza ute (mucous) na alkali za madini ya baikaboneti (bicarbonate ions) dhidi ya tindikali na kimeng’enya (enzyme) cha pepsini.
Mgawanyiko na utengenezwaji wa seli mpya za tabaka la juu la utumbo pamoja na uwepo wa damu ya kutosha ni baadhi ya vigezo vingine vinavyosaidia kulinda tabaka hili na utumbo dhidi ya kumomonyoka au kutoboka
Kuwepo kwa kigezo chochote kitakachoingiliana na ulinzi dhidi ya tabaka la juu la utumbo hupelekea kumomonyoka kwa tabaka hilo na kusababisha kidonda au vidonda vya tumbo ambavyo huweza kupelekea hata kutoboka kwa utumbo iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa
Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach ). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama
duodenum
Makundi ya vidonda vya tumbo
Kuna makundi makuu matatu ya ugonjwa huu-
A. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo ( Gastric ulcers).
B. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers).
C. Vidonda vinavyotokea kwenye koo
(Oesophageal ulcers)
AINA YA VIDONDA VYA TUMBO;
Kuna aina kuu mbili za vidonda vya tumbo;
1. gastric ulcers, Hii ni Aina ya kwanza ni ile inayoathiri tumbo
2. peptic ulcers, Aina ya pili ni ile inayoathiri utumbo mwembamba wa duodenam (duodenum ).
Hapo zamani ilikuwepo dhana kwamba msongo wa mawazo (stress) na mlo (diet) husababisha vidonda vya tumbo.Baadaye watafiti wa masuala ya afya ya binadamu waligundua
kuwa tindikali izalishwayo tumboni na vimeng’enya vya pepsini inachangia kiwango kikubwa katika kusababisha vidonda vya tumbo.
Lakinki hivi karibuni utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya asilimia themanini ya vidonda vya tumbo hutokana na bakteria aitwaye Heliocobacter pylori
(H.pylori). Ingawa inasadikika kwamba vigezo vyote hapo juu huchangia kupata vidonda vya tumbo,bakteria H.pylori anasadikiwa kuwa chanzo kikuu katika kusababisha vidonda vya tumbo.
a) VIDONDA VYA TUMBO (GASTRIC ULCERS) NA DALILI ZAKE
Asilimia kubwa ya waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo ni watu wenye umri zaidi ya miaka arobaini (40 ) na wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake.Waathirika wa aina hii ya vidonda vya tumbo huwa wembamba kutokana na kutokula wakihofia kupata maumivu pindi walapo chochote. Dalili kubwa ya wagonjwa hawa ni;-
· maumivu ya tumbo (chembe). Maumivu yake huwa yenye majira maalum ambapo huanza punde tu mgonjwa alapo chakula na hupungua baada ya chakula kuisha tumboni au kwa kunywa kimiminika chenye alkali.
· Hamu ya kula huwa nzuri lakini baadhi yao waweza kutapika .Kutapika damu (haematemesis) na kupata choo chenye damu (malaena) huweza kuambatana na aina hii ya vidonda vya tumbo.
· Uzito wa mwili hupungua kwa kiasi fulani kutokana na kutokula vizuri .
· Kusambaa kwa maumivu mpaka mgongoni kwaweza kutokea iwapo kidonda kimetoboka na kuhusisha kongosho (pancreas ).
b) VIDONDA VYA UTUMBO MDOGO (DUODENAL
ULCERS) NA DALILI ZAKE
Aina hii ya pili kwa upande mwingine huathiri watu wenye umri chini ya miaka arobaini (40) na kama aina ya kwanza,waathirika wengi ni wanaume.
· Maumivu yana tofauti na aina ya kwanza, hutokea kati ya masaa mawili na nusu hadi manne bada yamlo ambapo chakula huwa kimeisha tumboni ( hunger pains)
· . Maumivu pia hutokea zaidi mapema
asubuhi au nyakati za jioni .Nafuu hupatikana kwa kula chakula.
· Kutapika hutokea kwa nadra sana kwa wagonjwa wa aina hii.
· kutapika damu na kupata choo chenye damu hutokea mara nyingi zaidi kuliko aina ya kwanza .
· Hamu ya kula kwa wagonjwa wa aina hii huwa nzuri na hupenda kula mara kwa mara hivyo huwa na miili yenye afya nzuri tofauti na wagonjwa wa aina ya kwanza.
VISABABISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo husababishwa na
i) Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo ( gastric ulcers ) na zaidi ya asilimia 90 ya
duodenal ulcers.
Jinsi H.pylori anavyosababisha vidonda vya tumbo
Kuathirika na vimelea vya H.pylori ni kawaida kwa mwanadamu yeyote. Takwimu za Uingereza zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia hamsini ya idadi ya watu wazima wameathirika na bakteria hao.Idadi ni kubwa, zaidi ya asilimia tisini, kwa baadhi ya nchi nyingine.
Hata hivyo ni baadhi tu ya watu kati ya walioathirika na vimelea vya bakteria hawa hupata vidonda vya tumbo. Hakuna sababu za kisayansi zinazoelezea hali hiyo
Vimelea vya H.pylori huweza kusambaa kupitia chakula na maji.Vimelea vya bakteria hawa pia hupatikana kwenye mate hivyo vyaweza kuambukizwa kupitia kinywa haswa iwapo mtu
atabusiana na muathirika wa vimelea hivyo.Watu wengi pia huathirika na vimelea hivi utotoni.
Vimelea vya H.pylori huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana.Hapo hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho ambayo hupunguza makali ya
tindikali izalishwayo na tumbo yaani gastric juice/acid.Ili kukabiliana na hali hii,tumbo hutengeneza tindikali nyingi zaidi ambayo huathiri tabaka la juu la utumbo.Vimelea hivi pia hudhoofisha ute ulindao tabaka la juu la utumbo hivyo kushindwa kulinda tumbo na utumbo mwembamba sawasawa.
Aidha,vimelea vya H.pylori hujiegesha kwenye seli za tumbo.Hali hii hudhoofisha mfumo wa ulinzi wa tumbo na kusababisha maumivu na hatimaye madhara katika eneo lililoathirika.
Kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis ), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin , ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.
Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali ( gastric acid ) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama
Parietal cells . Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia huharibika, na hivyo
kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
ii)Matumizi ya dawa muda mrefu .
Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo ( gastric acid ) kwa kuwa na utando laini ( mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama
Prostaglandins . Dawa mfano za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.
iii)Uvutaji wa sigara:
Uvutaji sigara huchangia kutokea kwa vidonda vya tumbo kwa kiasi fulan,maana sumu ya nikotini na cafein iliyomo ndani ya sigara huamsha uzalishwaji wa tindikali ya gastric kwa wingi na kusababisha kiwango cha tindikali kuwepo kwa wingi tumboni hali ambayo husababisha ukuta wa utumbo kubabuka/kuchubuka
Iv)Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu:
Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo..
v)Unywaji wa pombe:
Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya
Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
vi)Vitu vingine:
Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeries ), kuungua kwa moto ( burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.
vii) Msongo wa Mawazo
Msongo wa mawazo hausababishi vidonda vya tumbo badala yake huongeza maumivu
kwenye kidonda kilichopo .Hufanya hivyo kwa kuongeza zaidi utengenezwaji wa tindikali tumboni
Viii) Kafeini (Caffeine)
Kafeini ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vinywaji kama soda, kahawa n.k huchangamsha utengenezaji wa tindikali tumboni ambayo huchubua ukuta wa utumbo na pia hutonesha kidonda kilichopo kama mtu ni mwathirika tayari.
VIASHIRIA VYA VIDONDA VYA TUMBO
i) Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda
wa kula chakula . Mtu mwenye vidonda kwenye
tumbo ( gastric ulcers ) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ( duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.
ii) Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.
iii)Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.
iv)Kichefuchefu na kutapika
v) Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
vi) Kutapika damu ,hii hutokea mara nyingi kwa watu wenye vidonda vilivyoko kwnye mfuko wa chakula(gastric ulcers)
vii)Kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia yenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali
NB:-
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa kwa muda muda mrefu bila
kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo .
Ni vyema kumuona daktari ili ufanyiwe uchunguzi na kupatiwa tiba sahihi iwapo una dalili zilizotajwa hapo juu. Pia ni muhimu kuzingatia dozi kwa kunywa dawa katika muda uliopangwa na kumaliza dozi hata baada ya dalili (maumivu) kupotea.
Ugonjwa wa vidonda vya tumbo tofauti na inavyodhaniwa waweza kupona kabisa kama magonjwa mengine.
Madhara kama kutoboka kwa utumbo,kuvuja damu, kuziba kwa tumbo na saratani ya tumbo yanaweza kutokea iwapo tiba haitatolewa katika muda muafaka.
MADHARA YA VIDONDA VYA TUMBO
Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kukumbwa na madhara yafuatayo;-
Ø Constipation , yaani kufunga choo au kwenda choo kigumu kama cha mbuzi.
Ø Kukonda/Kudhoofika , hii husababishwa na tumbo kushindwa kusaga chakula kwa kuwa kuna vidonda.
Ø Saratani ya utumbo , pia hii hujitokeza endapo vidonda vitakomaa na kuoza.
Ø Bawasiri/ au mang’ondi , hii husababishwa na viuvimbe vinavyoletwa na mdudu HB.
Ø Tumbo kuuma mara kwa mara kama typhoid, amiba na minyoo
USHAURI KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
1. Kula chakula kila baada ya masaa matano hadi sita, kumbuka usile kitu chochote katikati ya muda huo, mfano kama asubuhi umekula saa mbili, unaongeza mbele masaa matano au sita.
2.kunywa maji nusu saa kabla na baada ya mlo, kumbuka maji vuguvugu yafaa zaidi.
3.Epuka kutumia vitu vya baridi, vilivyolala na vya kwenye friji
4.Usitumie vitu vikali kama vile pilipili, limao, tangwizi, n.k
5.Kuwa na ratiba ya chakula isiyobadilikabadilika, ni muhimu kuwa na ratiba ya chakula isiyobadilika(fixed timetable).
6.kunywa maji glasi mbili mara baada ya kuamka na kila baada ya masaa mawili au mara usikiapo njaa.
7.Usitumie vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau, kwani huumiza tumbo.
8.Usiweke vyakula vya aina nyingi kwenye mlo mmoja, na matunda yasitumike pamoja na mboga za majani.
9.fanyamazoezi ya mara kwa mara asubuhi najioni, ususani mazoezi ya asubuhi kulifanya tumbo lako kufanya kazi vyema.
10.epuka kula chakula usiku sana au mida karibu na kulala.
HUDUMA YA KWANZA
1. Tumia juisi ya papai lililosagwa vizuri kila uonapo maumivu au ifanye kama desturi yako ili kuepusha maumivu makali ya tumbo.
2. Tumia maji ya vuguvugu pamoja na asali glasi moja kila baada ya masaa manne, na ifanye kama desturi yako.
3. Kama tumbo limekusababishia kuhara na kutoa damu chukua mkaa saga weka kwenye kikombe, tia na limao kidogo kunywa na m aji moto
LISHE KWA AJILI YA VIDONDA VYA TUMBO
v CHARDANS FOOD
Hii ni lishe nzuri sana kwa wale ambao matumbo yao yanashindwa kumeng’enya chakula vizuri na kujikuta wanapata kilungulila baada ya kula.
Mahitaji
§ Kilo moja ya viazi mbatata
§ Mimea miwili ya vitunguu
Maandalizi
ð Osha viazi vyako usivimenye
ð Vikate viazi vyako katikati
ð Katakata majani ya vitunguu vyako na uweke kwenye dishi
ð Tia viazi na chumvi ndani ya dishi pamoja na vitunguu
ð Chemsha kwa pamoja kwa joto la nyuzi 220
ð Kisha toa tayari kwa matumizi.
Nb;- hii lishe inasidia tumbo, na kusaidia moyo usipate high blood pressure, na kusaidia kutoa sumu kwenye figo.
v FRUIT SALAD
Hii ni lishe safi sana inalisaidia tumbo kuua vijidudu, vya minyoo, amiba, homa ya matumbo, UTI, pia husaidi kutoa mafuta mwilini
Mahitaji
§ Limao
§ Vitunguu swaumu na maji
§ Karoti
§ Tango
Maandalizi
ð Vioshe vyote kwa maji moto
ð Menya limao kisha katakata vipande, usitoe mbegu
ð Katakata vitunguu vipande vidogo vidogo
ð Katakata karoti na tango vipande vidogodogo bila kuvimenya
ð Changanya vyote kwenye sahani
Matumizi
Ø Tumia walau vijiko nane kutwa mara mbili kila baada ya masaa nane
Ø Mara umalizapo kutumia usinywe maji wala kula chochote mpaka baada ya dakika 45.
TIBA YA ULCERS
Matibabu ya tatizo hili uchukua takribani wiki sita hadi wiki ishirini na nne, hivyo mgonjwa wa namna hii ni vema akifika kituoni, apimwe ili kusudi tujue kuwa, vidonda ni vya aina gani na vipo katika hatua ipi.
Wengi wanadhana potofu kichwani mwao kuwa mtu hawezi kupona vidonda vya tumbo, mimi nakubaliana nao, kuwa ni kweli huwezi kupona kwa kuwa hauwezi kuzingatia kanuni za afya, lakini kwa wale wanaozingatia kanuni za afya kupona ni haraka na rahisi, njoo uwe shuhuda kwa wengine.
JAMB O MUHIMU KWETU
Kujua jinsi ya kujikinga na tatizo ni vyema sana kuliko kujua namna ya kujitibu, hivyo ni vyema turejee kwenye kanuni ambazo Mungu mwenyewe alituwekea kwa ajili ya uponyaji wa afya zetu kwani anahitaji tuwe wazima kimwili na kiroho, ndugu yangu hebu chukua hatua na uzingatie kanuni za afya ambazo ni;- hewa safi, maji safi, lishe bora, pumziko, mazoezi, mwanga wa jua, kiasi na kumtegemea MUNGU.
Kwa maswali na maoni kuhusu afya yako kwa ujumla swali tembelea
Email lovelinical05@gmail.com
Instagram
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni