KAMA UNA NDOTO ZA MAFANIKIO HAZIJATIMIA KWA SABABU YA KIPATO
CHAKO KIDOGO
SOMA HII MAKALA.
IMEANDALIWA NA DR LOVE
Njia rahisi za Kufanikiwa kwa kutimiza vitu vichache tu!!!!
Maisha yako ya mafanikio huanzia pale unapobaini katika maisha matamanio yako na kufanyia
kazi mipango yako kila siku iendayo kwa mungu pia kuchukia maisha unayoishi nayo kwa sasa
na kujuta kwa kuanza kujituma na kuweka bidii.
Mwanafalsafa mmoja aitwaye NAPOLEON HILL alisema "kutofanikiwa kwa watu wengi
kunatokana na watu wengi kushindwa kutengeneza mradi mwingine baada ya mradi wa
kwanza kushindwa kufanikiwa"
Mafanikio huhitaji uajibikaji na kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. Hapo tu utakapo kubali
kutimiza ndoto zako ndipo maisha yako huanza kubadilika.
Kumbuka pia bado tu wana falsafa wanatuambia kila mtu aliye tajiri leo hii alikua masikini katika
idara hio na hata alikua haijui biashara hio. Lakini mungu alipo muonesha njia alitumia fursa hiyo
mpaka leo hii ni matajili.
Ewe rafiki yangu ndugu yangu baba yangu leo hii naomba usome kwa makini utabarika kimaisha
,kiuchumi, kimwili, kipesa, kiakili na kiroho pia. Ungana nami Dr Mkumbo katika makala zangu za
biashara na afya.
HATUA ZA KUTENGENEZA MALENGO YA MAFANIKIO
HATUA YA KWANZA
1.FIKIRIA KWA MAKINI UNATAKA VITU GANI KATIKA KILA NYANJA ZA MAISHA YAKO.
Ndugu yangu unapokua na shauku ya mafanikio hebu ondoa upweke na unyonge na jisikie mwenye
furaha na ambae uko safarini kuelekea mafanikio hvyo basi jisikie mwenye mda wa kutosha,mwenye
pesa,mwenye marafiki wengi na mwenye elimu ya kutosha kutimiza ndoto yako leo.
Zifuatazo ni nyanja nne tu ukitaka kutimiza ndoto zako lazima ziwe zimetimilika na umeridhika.
A.KIPATO
- Jiulize ni pesa kiasi gani unahitaji kuzalisha mwaka huu,mwaka ujao, na miaka mitano ijayo.
-Je kipato chako kinakidhi malengo hayo???
B. FAMILIA.
-Je kipato hicho kinakidhi mahitaji yako na familia yako??
C.AFYA
- Je afya yako unaweza kuitunza na kuimarisha kwa kipato chako???
D.AKIBA
-Je ni pesa kiasi gani ungependa kujiwekea akiba kila siku,wiki,mwezi au mwaka??
-Je kipato chako unaweza kutumia na kubakiza ya kuweka akiba??
ZINGATIA:
-Watu wengi sana tumekata tamaa na maisha katika kushindwa kutimiza hio ndoto mpaka wengi
tukashindwa hata kufuata misingi ya kidini na kujiingiza katika mambo ya miujiza ili upate mali. Leo
hii rafiki yangu jua kwamba katika kutafuta mali hakuna miujiza ni uwezo tu wa kutumia akili yako na
kuwa na matamanio ya kufanikiwa na kuongea na walio juu yako ya mafanikio.
Napenda kuwapa ushuhuda wangu ,Nilipo kuwa form one nilikua napenda sana kumshirikisha Ndugu
Mwl. MGEMA ambae alikua ananipa mwanga wa mafanikio na kuona kuwa kumbe kufanikiwa darasani
haijalishi umesoma shule gani bali juhudi na matamanio pia kufuata ushauri ndio ngao ya mafanikio.
Napenda kumshukuru sana Mwl wangu huyu kwani mpaka sasa ndio ngao na mshauri wa mambo
yangu nina amini bado anamchango mkubwa katika maisha yangu kwani ndo alie nipa changamoto
hadi leo niko hapa naongea nanyi na niko na hatua kubwa ya Mafanikio. Mungu akuzidishie siku za
kuishi amina.
Wengi wana amini kukaa ndani na kuwa unacheka na marafiki wako wawili tu wakitalajia kufanikiwa.
Ndugu mafanikio hayaji hivi hivi umekaa kwako!!! Ongea na jamaa na marafiki kwa kuhudhuria
mikutano mbalimbali ya kiafya, kielimu ,kidini au kisiasa kuwa miongoni mwa hayo utapunguza hata
hatari ya kupata magonjwa tabia.
HATUA YA PILI
WEKA MALENGO YKO KATIKA MAANDISHI
- Inasemekana kuwa ni asilimia 3 tu ya watu wazima huandika malengo yao katika karatasi na
kuyafanyia kazi na asilimia 97 hawa hufanya kazi zao bila maandishi. Ndio maana ni watu wachache
tu hapa duniani ndo wanaofanikiwa na hawa wote ukiangalia wana mianya mingi ya kutoka kimaisha
kwani wanahudhuria semina mbalimbali ndani na nje ya nchi. Ewe kijana kila kongamano linadumisha
mila, desturi ,uchumi, udungu, na ajira hivyo anza kuhudhuria kuanzia leo.
HATUA YA TATU
WEKA TAREHE YA KUTIMIZA NDOTO ZAKO NA MIPANGO YAKO.
Kuna faida kubsa sana ya kuweka tarehe ya mwisho wa malengo yako kutimia hii itakupa nguvu ya
kifikra na hamasa ya mafanikio na woga wa kuzifikia hizo tarehe bila mafanikio. Hivyo njia hii
inakuongezea utendaji kazi wako sana ili kufikia mafanikio.
HATUA YA NNE
BAINI NA AINISHA VIPINGAMIZI UNAVYOTAKIWA KUVISHINDA ILI KUTIMIZA NDOTO ZAKO.
-Kaa chini chukua karatasi na kalamu andika vikwazo vyote unavyohisi ni vigezo vya wewe
kutokufikisha katika dunia ya mafanikio ili uanze kuandaa mbinu za kuziepuka.
Utafiti unaonesha kuwa asilimia 80 ya sababu zinazokurudisha nyuma kutimiza ndoto na malengo
yako ziko ndani ya nafsi yako. Na asilimia 20 tu ya vikwazo vinavyo kurudisha nyuma katika
mafanikio viko nje ya uwezo wako.
Hvyo unapo ainisha vikwazo anza na vikwazo vya ndani ya nafsi yako.
HATUA YA TANO
BAINI NA AINISHA UELEWA UBUNIFU NA TAARIF ZA NDANI ZAIDI KUHUSU MRADI UNAOTAKA
KUUFANYA.
-Watu wengi sana hata wasomi wakubwa huanzisha biashara wanashindwa kuendesha kwa sababu
wanafanya biashara kwa sababu Dr mkumbo anafanya .Unapotaka kuanzisha mradi wako au biashara
yoyote hebu kaa chini fikilia kwa undani kuhusu mradi wako na kubaini mbinu mbali mbali juu ya
mradi wako kutoka kwa mtu ambaye amefanikiwa .
Hii ndo faida ya kuongea na watu walioko mbele yako kiuchumi kielimu na kifikra na wala sio kujenga
chuki huwezi jua anaweza kua yeye ndo nyota ya asubuhi kwako. Mtu aliefanikiwa ndo atakae kupa
maelezo ya mradi,ujuzi na mbinu za kibiashara.
HATUA YA SITA
BAINI NA ORODHESHA WATU AMBAO NI MSAADA KWAKO KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO.
Ningependa kuwaambia kuwa kila mtu ana mchango wake katika miradi yetu hvyo usibague mtu kwa
kujali dini,kipato, kazi na elimu.
Unapofanya hili zoezi anza na ndugu yako wa karibu yani mama,baba,wajomba ,babu,bibi na wadogo
zako. Basi pia marafiki,majirani kwani hawa pia wana mchango mkubwa kwako pia ndo wateja wako.
Mimi nilianza kumshirikisha bibi yangu kipenzi na mlezi wangu ambae ndo mshauri wangu mkuu
kwani hunipa motisha katika mambo mazuri na yenye mafanikio Hivyo na wewe anza kushirikisha
ndugu yako wa karibu usianzishe mradi bila ndugu kujua kwani hao ndo wanaweza kuwa wateja
wakubwa kwako ndipo wakafutiwa na wengine.
HATUA YA SABA
ORODHESHA VITU VYOTE UNAVYOTAKIWA KUFANYA ILI KUTIMIZA MALENGO.
Hapa ndipo unatakiwa kuumiza kichwa kama ndio silaha ya kubwa ya kupambana na adui masikini na
kumpata kipenzi pesa tunaemsumbukia.
Unachotakiwa kufanya ni hiki orodhesha vitu vyote vikiwemo vikwazo yani changamoto, ambazo
unatakiwa kuzitatua wakati wa safari yetu ya mafanikio.
HATUA YA NANE
BAINISHA MALENGO YAKO NA WEKA KIPAUMBELE KWA LENGO ZURI LITAKALO KUPELEKA
MAFANIKIONI HARAKA.
ZINGATIA:
- Utafiti unaonesha kuwa unapotumia asilimia 20% ya muda wako kupanga mafanikio unahitaji
asilimia 80% ya nguvu kazi kutimiza malengo yako.
Hivyo juhudi ni muhimu na inahitajika katika mafanikio.
HATUA YA TISA
WEKA RATIBA YAKO INAYO ONESHA NAMNA GANI ITATIMIZA NDOTO ZAKO.
HATUA YA KUMI
CHAGUA KITU KIMOJA KIZURI AMBACHO UNAHISI KITAKUPRLEKA HARAKA SEHEMU UNAYO TAKA.
HESHIMU RATIBA YAKO.
-Watu wengi hawafanikiwi kwa kujali kuongea mambo ambayo hayamfanyi asonge mbele kiuchumi
kifikra kiafya nk
Hivyo ukitaka kufanikiwa tumia mda wako vizuri kuwa bize fanya mambo yako nina imani utafika
kwenye mafanikio.
Nashukuru wewe uliechukua mda wako kusoma makala hii pia ungana nasi kwa makala zangu za
kiafya na biashara.
Wasiliana nasi: 0755007592
Instagram:loveclinical
Blog:
Loveclinical05@gmail.com
Next
This is the most recent post.
Previous
Taarifa za zamani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni