MKOROGO KWA MAMA MJAMZITO/ MAMA ANENYONYESHA!
Hii swala la mkorogo huwa lina niumiza sana napoona mama mjamzito/ mama anaenyonyesha anapokuwa anajichubua.
Inasikitisha urembo wa mama unakuja kuwa sumu na kuleta kifo kwa mtoto.Kwa hali ya kawaida fikiria unapaka cream inabadili rangi ,inamanisha inasumu kali sana na inaingia ndani ya mwili ,mwili huo huo ndani umebeba kiumbe ndani yake,lazima itamwadhiri anaweza kuzaliwa akiwa mzima ila ile sumu ikawa inamtafuna taratibu baadae ndio akaanza kuumwa!
Mkorogo unapakwa mwili mzima mpaka Kwenye matiti ,hayo hayo matiti ndio mama anamnyonyesha mtoto, Mtoto ananyonyeshwa sumu kutoka kwenye mkorogo mara ngapi kwa siku?
Natamani madaktari wa Tanzania wengekuwa wanafanya research za maradhi ya watoto kwa wingi zaidi,kujua watoto wangapi wanafariki au kupata maradhi sugu kama cancer kutokana na mkorogo wa wazazi!
Vitu kama hivi wazazi wengi wanaojichubua hawana elimu ya kutosha juu ya hizi creams jinsi gani zina adhiri afya za watoto!
Watoto wengi wanapoteza maisha bila wazazi kujua kama mkorogo ni chanzo!
Tag rafiki
#Pinga mkorogo kwa breastfeeding moms
#Pinga mkorogo kwa pregomamaz
#Piga mkorogo jali afya yako #jiamini uzuri sio mpaka uwe mweupe
By Dr Love kwa ushauri wasiliana nami kupitia simu namba 0755007592
Chapisha Maoni