“Kwanza anatakiwa kusikiliza #FursaKumi, lakini pili lazima ajitambue
yeye, bila Nyota Ndoto kujua yeye ni mwanamuziki mzuri au ana kipaji
cha kuimba leo isingefikia hatua ya msanii Nyota Ndogo kutoka, nadhani
kikubwa wengi tunakosa kujitambua, kutojua tuna nini nguvu yetu ipo wapi
naamini kila mtu ana kipawa na ‘talanta’ aliyozaliwa nayo “Alisema Ruge
Mutahaba.
“Wengi hatujui ‘talanta’ tulizozaliwa nazo, kuna mtu anajua kuchora
vizuri lakini hajawahi kufikiria kuwa ni ‘designer’ mzuri kwa sababu
hakuna mtu aliyemsaidia kumwonyesha anaunganishaje hivi vitu ni kujaribu
kujifunza kujitathimini, kujifahamu” Aliongeza Ruge Mutahaba.
“Tunaona madalali, ni madalali wa nyumba wangapi wanatumia
‘Instagram’ kufanya biashara zao, shughuli zao za kazi zote
tunazozungumza ziko kwenye ‘contacts’ za simu, kwa kweli wanafanya kazi
nzuri sana, ‘smart phone’ inafanya kila kitu kwa sasa hivi” Ruge
Mutahaba
FURSA KUMI:
Fursa Namba 1: Biashara kwenye sekta ya Kilimo (Agri business).
Kilimo ndio msingi wa kila kitu, Watanzania wengi wanalima ili wapate
chakula ila si kwa ajili ya biashara. Jambo hili linatoa nafasi kwa watu
kuweza kuwekeza kwani kupitia Kilimo tutakuwa na viwanda na watu wengi
wataweza kujiajiri.
Fursa namba 2: Biashara ya Chakula (Food Business).
Fursa hii naitazama kwenye kuongeza dhamani katika biashara na kuzidiwa
kujitangaza, usipike tu kwa kawaida, ila ifanye kwa utofauti ikue na
kuongeza kipato.
Fursa Namba 3: Biashara katika sekta ya Mauzo, Manunuzi ya rejareja na Usambazaji kupitia njia ya mtandao (Retail – E commerce).
Unaweza kutumia mitandao kuuza bidhaa zako na kununua pia. Sio lazima
ukutane na mteja ana kwa ana ila kupitia mtandao unaweza kuanza nguo,
viatu na vitu vingine.
Fursa namba 4:Biashara katika tasnia ya Habari na Burudani(Media&Entertaiment.
Tukiweza kutengeneza film bora zitasaidia kufikisha tasnia hii mbali.
Nigeria wamerekodi filamu moja Marekani, ndani ya mwezi mmoja imeuza
kopi laki 5. Na wakati wa sisi kuwekeza zaidi na zaidi ili tufikie huko.
Fursa namba 5: Biashara kwenye sekta ya Huduma za Kijamii. Kwa sasa Tunaona Hospitali na Shule nyingi za binafsi na zinafanya vizuri sana. Hi ni nafasi kwetu kuwekeza.
Fursa Namba 6 :Biashara katika Tasnia ya Mitindo na Urembo
(Beuty &Fashion). zamani wote kwa mtazamo wetu mwonekano, mvuto
ulitokana na fahari ya mtu mwenyewe alichozaliwa nacho, lakini katika
ulimwengu wa sasa mwonekano wa mtu ni ‘featuring’ ya vitu vingi sana
kuanzia nywele, kucha, make up, fursa zipo nyingi mf. Sasa hivi unaweza
kuambiwa kufanya ‘pedicure & manicure’ ni shs elfu 40 hicho ni
kimoja tu”Ruge Mutahaba
Fursa Namba 7: Biashara ya Mashamba, Majengo/Mali isiyohamishika (Real Estate).
Tunaona Shule zinaongezeka na Vyuo pia. Hii inatoa nafasi kwa
Watanzania kuwekeza kwa kujenga Hostel ambazo zitatoa huduma kwa
Wanafunzi na ni kitu cha kudumu.
Fursa namba 8: Biashara katika sekta ya Usambazaji na Usafirishaji (Transport and Logistics).
Fursa namba 9: Sekta ya huduma za kifedha (Financial services) mfano ununuzi wa hisa. “Uelewa kuhusu masuala ya Hisa umekua sana na hii ni fursa nzuri sana kwa Vijana kama wataanza sasa kuwekeza katika Hisa”.
Fursa namba 10: Intaneti na Teknolojia. Mambo mengi
sana kwa sasa yanafanyika kupitia mitandao. Watu wanaweza kufanya
biashara kupitia mitandao Hii ni nafasi kwetu sisi kuweza kuwekeza. Hii
itatupa nafasi ya kujiajiri na pia kwenda na wakati
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni