Kila siku
asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti
ya Tanzania,
Moja habari zilizoandikwa ni hii habari kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari ‘Maziwa ya kopo ni hatari kwa watoto’
Wazazi na
walezi nchini wametakiwa kuacha kutumia maziwa ya kopo na ya Ng’ombe kwa
watoto ambao hawajafikisha mwaka mmoja ili kuwanusuru katika tatizo la
kuchubuka utumbo.
Ushauri
huo ulitolewa jijini Dar es salaam na kaimu mkurugenzi kitengo cha afya
ya uzazi na mtoto, Dk. Georgina Msemo, katika maadhimisho ya
unyonyeshaji yanaayoendelea.
Dk Msemo
alisema maziwa ya ng’ombe yana Casein ambayo haifai kwa mtoto mwenye
umri wa kuzaliwa hadi mwaka mmoja pia alisema maziwa hayo husababisha
mzio, pumu na kusema kwamba maziwa ya mama ni bora na yanayotoa kinga ya
mwili kwa mtoto katika maisha yake yote.
Chapisha Maoni